Idara ya Sheria Inasuluhisha Ukaguzi wa Haki za Kiraia za Mfumo wa Mahakama ya Umoja wa Dakota Kusini
Kumbuka: Taarifa hii kwa vyombo vya habari imetafsiriwa katika lugha mbalimbali. Angalia viambatisho vilivyo hapa chini.
WASHINGTON – Leo hii Idara ya Sheria imetangaza kwamba imetatua ukaguzi wa haki za kiraia za Mfumo wa Mahakama wa Umoja wa Dakato Kusini (UJS) ambao utawasaidia watu wenye ujuzi finyu wa Kiingereza (LEP) ili waweze kuwasiliana katika mahakama ya jimbo.
Ukaguzi wa Idara ya Sheria ulianza baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Huduma za Kisheria za East River ikidai kwamba mahakama za UJS ziliwabagua wafanyakazi wa mahakama wenye ujuzi finyu wa Kiingereza (LEP) kulingana na asili yao ya kitaifa ambayo ni kinyume cha Sehemu ya VI ya Sheria ya Haki za Kiraia ya 1964. Sehemu ya VI inakataza wanaopokea usaidizi wa kifedha wa serikali kuwabagua watu kwa sababu ya mbari, rangi au asili yao ya kitaifa. Ukaguzi wa idara ulitambua kwamba vizuizi vya lugha na gharama kubwa kwa mahakama ya UJS zinawazuia watu wenye ujuzi finyu wa Kiingereza yani LEP kushiriki katika kesi za kiraia na mashtaka.
“Mahakama ya jimbo ni msingi wa uadilifu wa mfumo wetu wa haki na ni muhimu kwamba vikwazo vyovyote vinavyowazuia watu kufikia taasisi hizi viondolewe,” alisema Msaidizi wa Mwanasheria Mkuu Kristen Clarke wa Idara ya Sheria Kitengo cha Haki za Kiraia. “Tutaendelea kushirikiana na mahakama za jimbo ili tuondoe vizuizi vya lugha vinavyowazuia watu kupata haki na vinavyokiuka sheria ya haki za kiraia ya serikali. Tunashukuru Mfumo wa Mahakama ya Umoja wa Dakota Kusini kwa kushirikiana na Idara ya Sheria ili kutatua jambo hili na kuchukua hatua ya haraka ya kuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wa mahakama wanaweza kuelewa na kushiriki katika kesi, bila kujali uwezo wao wa kuzungumza na kuandika Lugha ya Kiingereza.”
Kwa sababu ya ukaguzi wa idara, UJS ilianzisha mswada katika bunge la jimbo wa kuongeza wakalimani na watafsiri kwa ajili ya watu wenye ujuzi finyu wa Kiingereza yani LEP katika kesi zote za kiraia. Sheria hiyo iliyotungwa ilikuwa sheria mnamo Julai tarehe 1. Kwa ajili ya kutekeleza sheria hiyo mpya, UJS ilipata fedha za ziada katika bajeti yake za kutoa huduma za wakalimani za bure kwa watu na mashahidi wenye ujuzi finyu wa Kiingereza yani LEP. Isitoshe, UJS imesasisha mipango ya kupata huduma za lugha kwa ajili ya safari zote za kutembelea mahakama za jimbo, imeteua mratibu wa kupata huduma za lugha na imeunda mchakato wa malalamiko ya kupata huduma za lugha. Mratibu na taratibu za malalamiko zitasaidia katika kuhakikisha kwamba watu wanaweza kutoa maoni kwa UJS. UJS pia imekubali kuendelea kushirikiana na idara ili iendeleze haki na kutowabagua watu wenye ujuzi finyu wa Kiingereza yani LEP katika kufikia mahakama.
Kesi hii ilichunguzwa na mawakili wa Kitengo cha Haki za Kiraia pamoja na Ofisi ya Wakili wa Marekani wa Wilaya ya Dakota Kusini. Utekelezaji wa Sehemu ya VI ni muhimu sana kwa Kitengo cha Haki za Kiraia. Taarifa ya ziada kuhusu Kitengo cha Haki za Kiraia inapatikana kwenye tovuti yake www.justice.gov/crt, na taarifa kuhusu ujuzi finyu wa Kiingereza na Sehemu ya VI inapatikana kwenye www.lep.gov. Watu wanaweza kuripoti mambo yanayoweza kuwa ukiukaji wa haki za kiraia kwenye https://civilrights.justice.gov/report/ au kwa Ofisi ya Wakili wa Marekani wa Wilaya ya Dakota Kusini kwa kujaza fomu ya malalamiko inayopatikana kwenye https://www.justice.gov/usao-sd/civil-rights.