Skip to main content
Press Release

Idara ya Haki Inafunga Ukaguzi baada ya Mfumo wa Mahakama wa Dakota Kusini Kuboresha Ufikiaji kwa Watu Wenye Ustadi Kiasi wa Kiingereza

For Immediate Release
Office of Public Affairs

Idara ya Haki leo (The Justice Department) imetangaza kuwa itafunga ukaguzi wa haki za kiraia kulingana na hatua ambazo Mfumo wa Mahakama wa Dakota Kusini (Unified Judicial System, UJS) umechukua ili kuboresha ufikiaji wa mipango na shughuli za mahakama kwa watu wenye ujuzi kiasi wa Kiingereza (limited English proficiency, LEP).

Mnamo Oktoba 2021, Idara ya Haki ilitatua ukaguzi wa UJS uliofunguliwa kwa mujibu wa Title VI ya Sheria ya Haki za Kiraia ya 1964 (Title VI of the Civil Rights Act of 1964, Title VI), ambayo inakataza ubaguzi kwa misingi ya mbari, rangi na asili ya kitaifa na wapokeaji wa usaidizi wa kifedha wa shirikisho. UJS imechukua hatua kadhaa ili kuboresha watu wa LEP kufikia mahakama za serikali huko Dakota Kusini. UJS pia imerasimisha mpango wa kufikia lugha ya mahakama, na hivi majuzi, UJS ilitoa mpango wa ufikiaji wa lugha katika jimbo lote ambayo inahitaji mahakama zote kutoa huduma za mkalimani na mfasiri bila gharama kwa watumiaji wa mahakama ya LEP. Zaidi ya hayo, UJS imewapa majaji na wafanyakazi wa mahakama ufikiaji wa mafunzo ya lugha ambayo inashughulikia Title VI na mahitaji ya sheria ya serikali. Idara inafunga ukaguzi huu kutokana na juhudi hizi na nyinginezo za UJS.

"Lugha haipaswi kuwa kama kizuizi kwa watu wanaotafuta haki na ufikiaji wa mahakama katika nchi yetu," alisema Msaidizi wa Mwanasheria Mkuu Kristen Clarke wa Kitengo cha Haki za Kiraia cha Idara ya Haki (Civil Rights Division). "Tunatambua maboresho ya Mfumo wa Mahakama wa Dakota Kusini ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha ufikiaji wa mahakama za serikali kwa watu ambao wana ustadi kiasi wa kiingereza."

"Kutoka kwa mswada wa UJS uliowasilishwa mwaka jana ambao ulikuwa sheria ya serikali hadi mpango wa hivi majuzi wa ufikiaji wa lugha, UJS imeboresha uzoefu wa watumiaji wa mahakama ya LEP katika jimbo letu," alisema Wakili wa Marekani Alison J. Ramsdell wa Wilaya ya Dakota Kusini. "Ofisi yetu imejitolea kufanya kazi na washirika wa serikali na wa mtaa kushughulikia ufikiaji wa lugha na maswala mengine muhimu ya haki za kiraia."

Suala hili liliendeshwa kwa pamoja na wanasheria katika Kitengo cha Haki za Kiraia na Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani katika Wilaya ya Dakota Kusini. Maelezo ya ziada kuhusu Kitengo cha Haki za Kiraia yanapatikana kwenye tovuti yake kwa www.justice.gov/crt, na maelezo kuhusu ujuzi kiasi wa Kiingereza na Title VI yanapatikana katika www.lep.gov. Wanachama wa umma wanaweza kuripoti ukiukaji wa haki za kiraia unaowezekana katika https://civilrights.justice.gov/report/ au kwa Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani wa Wilaya ya Dakota Kusini kwa kujaza fomu ya malalamiko inayopatikana katika https://www.justice.gov/usao-sd/civil-rights.

Updated May 28, 2023

Topic
Civil Rights
Press Release Number: 22-866